Latest News & Events

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA NANE WA MWAKA

Kutakua na Mkutano Mkuu wa Mwaka (8th AGM) wa Chama cha Wakandarasi Wazawa siku ya Jumatano na Alhamisi ya 24 na 25 Aprili 2019 utakaofanyika katika Ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel (Ledger Plaza), Dar es Salaam

MUDA: Kuanzia Saa Mbili kamili Asubui hadi Saa Kumi jioni

KAULI MBIU: Uendelefu wa Biashara ya Ujenzi nchini Tanzania- Jinsi ya kuboresha mazingira ya Biashara
MGENI RASMI: Tunatarajia kua na Katibu Mkuu- Wizara ya Ujenzi

WANACHAMA WOTE NA WAGENI WAALIKWA KUHUDHURIA BILA KUKOSA.

KWA MAWASILIANO, PIGA SIMU: 0762 074441 AU TUMA BARUA PEPE INFO@ACCT.CO.TZ

BI. ANGELA JOSEPH
KATIBU MTENDAJI- ACCT

SEMINA YA NAMNA YA KUANDAA ZABUNI ZENYE UFANISI KATIKA SEKTA YA UMMA

Chama cha Makandarasi wazalendo (ACCT) inakualika kwenye Semina inayolenga kumjengea mkandarasi uwezo katika nyanja mbalimbali za ujazaji na ushindani wa zabuni, ujazaji wa gharama inayotekelezeka katika kufanya mradi, utekelezaji na usimamizi wa mkataba wa mradi, vitu vinavyopaswa kufanyika na visivyopaswa kufanyika wakati wa kuandaa zabuni, na mikakati mbalimbali inayoweza kutumika ili kuweza kushinda zabuni.

Mada: Namna ya kuandaa zabuni zenye ufanisi katika sekta ya Umma "Preparing Successful Tenders for the Public Sector"

Ada ya Ushiriki: Wanachama ni Tsh. 300,000/= na kwa wasio Mwanachama ni Tsh. 350,000/= kwa kila mshiriki

Tarehe: 16 & 17 August, 2018 (Alhamis & Ijumaa)

Muwezeshaji “Facilitator”: Dr. Ramadhan Mlinga

Mahali: Dar -es -Salaam.

Wanaopaswa kuhudhuria: Semina hii inawalenga Makandarasi, Washauri, Maafisa ununuzi, Maafisa ugavi na wadau wote wa sekta ya ujenzi wanaalikwa kuhudhuria ili kuweza kujifunza na kuongeza uelewa zaidi katika tasnia hii.

Makandarasi wote mnakaribishwa kushiriki, Tafadhali thibitisha uwepo wako kupitia Email : info@acct.co.tz, au piga simu 0762 074 441.
Pia tunakaribisha wadhamini kutumia fursa hii kwa ajili kutangaza biashara zao.