Chama cha Makandarasi wazalendo (ACCT) inakualika kwenye Semina inayolenga kumjengea mkandarasi uwezo katika nyanja mbalimbali za ujazaji na ushindani wa zabuni, ujazaji wa gharama inayotekelezeka katika kufanya mradi, utekelezaji na usimamizi wa mkataba wa mradi, vitu vinavyopaswa kufanyika na visivyopaswa kufanyika wakati wa kuandaa zabuni, na mikakati mbalimbali inayoweza kutumika ili kuweza kushinda zabuni.
Mada: Namna ya kuandaa zabuni zenye ufanisi katika sekta ya Umma "Preparing Successful Tenders for the Public Sector"
Ada ya Ushiriki: Wanachama ni Tsh. 300,000/= na kwa wasio Mwanachama ni Tsh. 350,000/= kwa kila mshiriki
Tarehe: 16 & 17 August, 2018 (Alhamis & Ijumaa)
Muwezeshaji “Facilitator”: Dr. Ramadhan Mlinga
Mahali: Dar -es -Salaam.
Wanaopaswa kuhudhuria: Semina hii inawalenga Makandarasi, Washauri, Maafisa ununuzi, Maafisa ugavi na wadau wote wa sekta ya ujenzi wanaalikwa kuhudhuria ili kuweza kujifunza na kuongeza uelewa zaidi katika tasnia hii.
Makandarasi wote mnakaribishwa kushiriki, Tafadhali thibitisha uwepo wako kupitia Email : info@acct.co.tz, au piga simu 0762 074 441.
Pia tunakaribisha wadhamini kutumia fursa hii kwa ajili kutangaza biashara zao.